Loading...
Nyota wa timu ya taifa ya soka ya Brazil na klabu ya Paris Saint-Germain Neymar aliripotiwa kuchagua Arsenal na Chelsea kama vilabu vya pekee vinavyoweza kumvutia kuhamia Uingereza ikiwa ataondoka kwenye klabu yake ya sasa.
Kwenye msimu wa uhamisho uliopita, Neymar alihusishwa na uhamisho kuelekea Manchester City ambapo alisemekana kufurahia kupata nafasi ya kucheza chini ya mkufunzi Pep Guardiola.
Hata hivyo, kulingana na jarida la Express UK, nyota huyo wa zamani wa Barcelona anapenda sana jiji la London na yuko radhi kujiunga na Chelsea au Arsenal.
"Anapenda Uingereza, lakini hasa London. Amekuwa humo mara tatu au nne kwa miezi 12 iliyopita. Anasema kuna kitu kizuri kuhusu London.
"Mara ya mwisho, alinipigia simu mara kadhaa na kuniomba kujiunga naye kwa kuwa alilipenda jiji hilo. Alisema mara nyingi kuwa eneo hilo ni nzuri. Anapenda London," Chanzo cha habari karibu na Neymar kiliyafichua hayo kwa Express UK.
Msimu huu, Neymar ameonyesha mchezo mzuri akiwa PSG iliyo kwenye ligi ya Ufaransa, akifunga mabao matatu kwa mechi nne alizocheza.
Hapo awali, iliripotiwa kuwa Manchester United iliwasiliana na nyota huyo wa Brazil kuhusu uhamisho kuja Old Trafford.
Licha ya kuhamia Ufaransa mwaka uliopita, Neymar amehusishwa na uhamisho wa kuondoka PSG.
Na Hamisi Mchuka.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
NEYMAR AFICHUA TIMU MBILI ZA EPL ZINAZOWEZA KUMSHAWISHI KUHAMIA UINGEREZA
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
9/03/2018 12:03:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: