Loading...
Rapa T-Pain akamatwa na polisi katika uwanja wa ndege wa Atlanta, Georgia baada ya mlinzi wake kukutwa na bastola ndogo wakati wa ukaguzi wa mizigo.
Wote wawili rapa huyo na mlinzi wake walizuiliwa kituoni hapo kwa ajili ya uchunguzi zaidi mpaka polisi watakapo jiridhisha, ndipo baadae iligunduliwa kuwa rapa T-pain ndio mmiliki halali wa bastola hiyo na bunduki ikarudishwa kwa rapa huyo.
Na ndipo wawili hao wakaachiliwa kutoka kizuizini na hakukua na kesi yeyote iliyofunguliwa. Ijapokuwa, waliambiwa uchunguzi unaendelea ili kuangalia kama mlinzi wake atafunguliwa mashtaka kwa kumiliki bastola katika sehemu ya ukaguzi wa mizigo.
Na Neema Joshua.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
RAPA T-PAIN AKAMATWA KWA KUKUTWA NA BUNDUKI
Reviewed by By News Reporter
on
9/01/2018 04:15:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: