Loading...
Maafisa wa polisi wanafanya uchunguzi kuhusiana na kifo cha mmoja wao ambaye alifariki katika hali tatanishi mjini Malindi - Kenya, Ijumaa Agosti 31.
Kulingana na afisa mmoja kutoka kituo cha polisi cha Malindi, marehemu alikuwa akihudumu katika kaunti ya Lamu na alifariki baada ya kunywa pombe kwa siku mbili mfululizo.
OCPD wa Malindi Matwa Muchngi alidhibitisha kisa hicho na kusema kuwa alishangazwa sana ni vipi afisa huyo aliamua kunywa pombe nyingi bila ya kula chochote.
Matwa alisema kuwa afisa huyo alikuwa safarini kutoka Lamu akielekea Malinda ila aliamua kujiburudisha kidogo mjini Malindi.
OCPD huo aliongezea kwamba huenda afisa huyo alikuwa na matatizo ya kinyumbani au msongo wa mawazo, kiini kikuu kilichompelekea kunywa kupita kiasi.
Mwili wa mwendazake ulisafirishwa hadi mjini Nairobi na taarifa zaidi itatolewa baada ya uchunguzi kumalizika.
Na Yohana Mussa.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
VISA NA MIKASA: AFISA POLISI AFARIKI DUNIA KWA KUNYWA POMBE SIKU 2 MFULULIZO
Reviewed by By News Reporter
on
9/01/2018 02:30:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: