Loading...

WANANDUGU WABAINI BINTI YAO YUPO HAI BAADA YA KUDAIWA AMEFARIKI

Loading...
Ndugu wabaini binti yao yupo hai muda mfupi baada ya kukabidhiwa mwili wa binti huyo kwa hatua za mazishi ikiwa ni baada ya daktari kuthibitisha kifo chake.

Binti huyo, Selina Michael(17) mkazi wa mtaa wa Butunga alipelekwa katika hospitali ya Baptist kupata matibabu na baadae familia kuarifiwa na Mganga wa zamu kuwa binti huyo amefariki.

Wazazi wa binti huyo wameeleza kuwa chanzo cha binti huyo kupelekwa hospitali ni baada ya kuanguka ghafla alipokuwa akishuhudia vurugu zilizokuwa zikiendelea nyumba ya jirani.

Aidha, Mganga Mkuu Mfawidhi wa hospitali hiyo, James Chausa amekiri kumpokea binti huyo na kwamba Mganga wa zamu wa siku hiyo Cassian Ndilaliha alimpima na kubaini kuwa tayari amekwishapoteza maisha.

Inadaiwa kuwa binti huyo alipoteza maisha kwa nguvu za giza na wakati daktari anampima hakuwa na mapigo ya moyo.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
WANANDUGU WABAINI BINTI YAO YUPO HAI BAADA YA KUDAIWA AMEFARIKI WANANDUGU WABAINI BINTI YAO YUPO HAI BAADA YA KUDAIWA AMEFARIKI Reviewed by By News Reporter on 9/01/2018 01:12:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.