Loading...
Familia moja ya kijiji cha Kiwani Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba, imetakiwa kurejesha fedha za mahari ilizopokea kwa ajili ya kumuozesha msichana anayesoma darasa la sita.
Mkuu wa Mkoa huo, Hemed Suleiman Abdalla, alitoa agizo katika mkutano alioufanya huko Kiwani ikiwa ni mfululizo wa ziara zake za kuangalia shughuli mbalimbali za maendeleo na kusikiliza kero za wananchi.
Mkuu huyo alisema anazo taarifa kuna familia imeshapokea mahari kwa ajili ya kumuozesha msichana anayesoma darasa la sita, hali ambayo itasababisha binti huyo kukosa haki yake ya msingi ya kupata elimu.
Aliagiza kurejeshwa fedha hizo na binti aendelee kusoma bila ya kuozeshwa hadi uwezo wake utakapofikia sambamba na kutaka hatua za kisheria zichukuliwe kwa waliopokea mahari hiyo.
Aidha mkuu huyo alitoawito kwa wananchi wa Kiwani kuacha tabia ya kuwalinda wahalifu katika maeneo yao na badala yake wawe tayari kushirikiana na polisi jamii kuzuia uhalifu kwa kutoa taarifa.
Na Zaida Msafiri.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
RC AAGIZA KURUDISHWA KWA MAHALI
Reviewed by By News Reporter
on
9/01/2018 12:44:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: