Wakali wa muziki wa Injili, Joel Lwaga wa hapa nchini na Chris Shalom kutoka Nigeria, wameandika historia baada ya kuachia kolabo yao ya "Umejua kunifurahisha".
Chris anayetamba na wimbo wa 'My Beautifier' na 'Power Belongs to You' na Joel Lwaga anayetamba na wimbo wa 'Utabaki kama Ulivyo' wametumia lugha ya Kiingereza na Kiswahili kwenye wimbo huo.
Akizungumza na gazeti moja la habari hapa nchini, Lwaga amesema wimbo huo wa ushuhuda na shukrani umebeba moyo wa mtu aliyepitia magumu ambayo asingeweza kustahimili na kuvuka bila msaada wa Mungu.
"Huu wimbo pia unatabiri mema juu ya maisha ya mtu anayepitia magumu wakati huu, ni wimbo wa baraka sana hivyo watu watarajie kuinuliwa mioyo yao,"

Loading...
alisema Lwaga.
Alisema kwamba kolabo yao inafungua ukurasa mpya ya wanamuziki wa injili wa hapa nyumbani na Nigeria katika kuandaa kazi za pamoja.
"Mimi nimeanza na Mungu amenitumia kama mfungua mlango, ni wakati wa muziki wetu wa injili kuvuka mipaka na kuwafikia watu wengi ulimwenguni," alisisitiza na kuongeza;
"Tumetumia pia lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa hiyo ni wakati wa lugha yetu kuendelea kusikika duniani kupitia kazi zetu za muziki," alisema.
Na Neema Joshua.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

JOEL LWAGA KATIKA KOLABO KALI NA MSANII WA NIGERIA
Reviewed by By News Reporter
on
9/29/2018 08:59:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: