Loading...

KISWAHILI SASA KUFUNDISHWA SHULE ZA MSINGI AFRIKA KUSINI

Loading...
Kuanzia 2020, lugha ya kiswahili itafundishwa katika shule za Afrika Kusini kama somo la hiari. Kwa mujibu wa Waziri wa Elimu ya Msingi Angie Motshekga, kuiniza Kiswahili kwenye mfumo wa elimu yetu utasaidia kuwaleta Waafrika pamoja.

Kiswahili kitakuwa lugha pekee ya Afrika, kutoka nje ya mipaka ya Afrika Kusini, kufundishwa kwa wanafunzi wa nchi hiyo.

Mfumo wa elimu ya Afrika Kusini unatoa fursa pia kwa kufundisha lugha za kigeni kama Kifaransa, Mandarin na Kijerumani kama masomo mbadala.

"Kiswahili ni mojawapo ya inayozungumzwa zaidi barani Afrika baada ya Kiarabu na Kiingereza; na inaweza kusambaa zaidi hata kwa nchi ambazo zilikuwa hazikizungumzi na hatimaye kuwaunganisha Waafrika pamoja," alisema Bi Motshekga.

Bi Motshekga aliongeza zaidi kuwa Kiswahili kuwa mojawapo ya lugha rasmi za Umoja wa Afrika, tukiondoa kila aina ya shaka lugha hii ya kiafrika itaendeleza ushirikiano wa kijamii kati ya Afrika Kusini na mataifa mengine ya Afrika.

Kwa makubaliano, kiongozi wa upinzani wa Afrika Kusini Julius Malema alisema kuwa kama Kiswahili ingeendelea kukuwa na kuwa lugha ya bara letu, basi Afrika itafanya hatua kubwa na kujikwamuwa na ukoloni daima.

Malema aliongeza kuwa wakati tunapokuwa na lugha inayounganisha Waafrika, basi tutaweza kuondokana na kuzungumza kwa lugha za kigeni kama vile Kiingereza.

Kiswahili ni lugha ya kitaifa nchini Kenya, Tanzania, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
KISWAHILI SASA KUFUNDISHWA SHULE ZA MSINGI AFRIKA KUSINI KISWAHILI SASA KUFUNDISHWA SHULE ZA MSINGI AFRIKA KUSINI Reviewed by By News Reporter on 9/20/2018 06:19:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.