Loading...
Taarifa ya awali ya BBC ilisema: "Mbunge wa Upinzani nchini Uganda Bobi Wine akamatwa na kulazimishwa kuingia gari la jeshi mara baada ya kuwasili Entebbe akitokea Marekani alikokwenda kusafanyiwa matibabu."
Hata hivyo maafisa wa polisi nchini humo wamekana madai ya kukamatwa kwa Kyagulanyi na kusema walikuwa wakimsindikiza nyumbani. "Hamna aliyemkamata Bobi Wine, tunamsindikiza tu," Inspekta Mkuu wa Polisi, Okoth Ochola alisema.
Ripoti zaidi zinasema kuwa, tayari umati ulikuwa umeanza kushuhudiwa katika kituo cha polisi cha Kasangati alikoaminiwa kuwa, huku maafisa zaidi wa usalama wakipelekwa katika boma la Mbunge huyo wa Kyadondo Mashariki Mashariki.
Ripoti za awali za BBC zilisema kuwa, Mbunge huyo alitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jumo Kenyatta (JKIA) jijini Nairobi, Alhamisi, Septemba 20, kabla ya kuendelea na safari yake kwenda Entebbe akitumia ndege ya shirika la Kenya Airways.
Pia ilidaiwa kuwa, Eddie Yawe, kaka yake Wine alitiwa nguvuni alipokuwa akielekea uwanja wa ndege kumlaki mwanasiasa huyo. Awali polisi walikuwa wameonya umma na mafuasiwa wa Bobi Wine dhidi ya kuandamana ama kuandaa mikutano ya kumkaribisha Wine.
Vyombo vya habari pia vilionywa dhidi ya kupeperusha moja kwa moja ujio wa mwanasiasa huyo.
Bobi Wine alisafiri kwenda Marekani kufanyiwa matibabu licha ya serikali kujaribu kumzuia na hii ilikuwa baada ya kukamatwa na kuzuiwa siku kadhaa na hata kushtakiwa kwa kosa la uhaini kwa madai alihusika na kupigwa mawe gari la Rais Yoweri Museveni.
Kukamatwa kwake kulizua hali tete mno nchini humo huku ghasia zikiripotiwa sehemu mbalimbali nchini Uganda.
Na Mwajuma Twaha.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

BOBI WINE AKAMATWA TENA BAADA YA KUWASILI ENTEBE
Reviewed by By News Reporter
on
9/20/2018 05:11:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: