Loading...
Kivuko cha Mv Nyerere kinachotoa huduma kati ya Bugorola na Ukara katika Kisiwa cha Ukerewe mkoa wa Mwanza kimezama.
Bado idadi kamili ya watu waliopanda haijafahamika bado kuwa kilikuwa kimebeba na abiria wangapi. Inadaiwa kuwa kilikuwa na abiria zaidi ya 100.
Shughuli za uokoaji abiria waliozama katika Kivuko cha Serikali cha MV. Nyerere kilichokuwa kikitoa huduma za safari ndani ya Ziwa Victoria kati ya Kisiwa Kikubwa cha Ukerewe na Ukara, kilichopinduka na kuzama leo, zimeanza ambapo hadi sasa zaidi ya watu 20 tu waliokuwa nje ya kivuko hicho wakining'inia, wameokolewa.
Sababu za awali za kuzama kivuko hicho inadaiwa kuwa ni idadi kubwa ya watu waliokuwa wamepanda pamoja na idadi kubwa ya mizigo ya magunia ya mahindi na mifuko mingi ya saruji.
Kivuko hicho cha MV Nyerere kilichokuwa kinachofanya safari zake kati ya Bugorora katika Kisiwa cha Ukerewe na Kisiwa cha Ukara katika Ziwa Victoria mkoani Mwanza kimezama leo Alhamisi Septemba 20, 2018.
Akizungumza na Mwandishi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shana amesema kivuko hicho kimezama wakati kikielekea katika Kisiwa cha Ukara.
“Ni kweli kivuko cha MV Nyerere kimezama kilikuwa kinatoka Bugorora katika Kisiwa cha Ukerewe kuelekea Kisiwa cha Ukara,” amesema.
Kamanda Shana amesema kuwa kivuko hicho kimezama leo mchana baada ya kulalia upande mmoja kupinduka na kupelekea kuzama.
“Kiliondoka saa 6 mchana na ilipofika saa nane kamili mchana kilipinduka,” amesema.
Amesema kuwa watu ishirini na watatu wameokolewa na shughuli ya uokoaji inaendelea ikiongozwa na mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella.
“Mpaka sasa kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na mkuu wa mkoa iko eneo la tukio lakini waliookolewa mpaka sasa hivi ni wachache, wengine bado wako humo wakiomba msaada,” amesema.
Amesema bado hawajapata idadi kamili ya waliokuwemo kwenye kivuko hicho.
Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), Hassan Karonda amekiri kuzama kwa kivuko hicho na yuko njiani kulekea huko na watatoa taarifa baadaye.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, Denis Kwesiga, kivuko hicho kimezama kikiwa mita 50 kutia nanga katika bandari ya Ukara.
Shuhuda huyo amesema kivuko hicho ambacho kinabeba abiria 101 na tani kadhaa za mizigo, hadi sasa zaidi ya watu 20 wameokolewa kutoka kwenye ajali hiyo na kupelekwa kwenye kituo cha afya cha Bwishe.
“Siku ya Alhamisi kivuko hicho huwa kinabeba abiria wengi na mizigo kwa sababu kisiwa cha Ukara huwa ni siku ya gulio hivyo kuna uwezekano wa watu wengi kuzama,” amesema Kwesiga.
Na Hamisi Maftah.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

HABARI ZA HIVI: KIVUKO CHA MV NYERERE CHAZAMA
Reviewed by By News Reporter
on
9/20/2018 04:56:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: