Loading...
Mwili wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, ambaye alifariki mwezi uliopita, umewasili katika nchi aliyozaliwa, Ghana.
Mwili wake uliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kotoka International Airport mjini Accra, ukisindikizwa na familia yake na maafisa wengine wa Umoja wa Mataifa.
Anatarajiwa kuzikwa kitaifa siku ya Alhamisi.
Kulikuwa na hali ya maombolezo wakati mwili wake ukiwasili uwanjani hapo na kupokelewa na Rais wa Ghana Akufo Addo na viongozi wa kimila na kwa heshima ya kijeshi.
Mwili wake umehifadhiwa katika Ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Ghana, wakati ukisubiri kuzikwa.
Kofi Annan alikuwa ni Katibu mkuu wa kwanza wa Umoja wa Mataifa, kutoka katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara na kuleta mafanikio sio tu katika bara la Afrika, lakini pia dunia nzima.
Aliwahamasisha vijana wengi nchini mwake na waliheshimu kile alichosimamia.
Na Paskali Joseph.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
KOFFI ANNAN KUZIKWA GHANA ALHAMISI WIKI HII
Reviewed by By News Reporter
on
9/11/2018 07:59:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: