Loading...
Mahakama ya kimataifa ya mjini The Hague, ICC, imemhukumu mwanasiasa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jean-Pierre Bemba faini ya dola laki tatu na kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kuvuruga ushahidi.
Hata hivyo, Bemba hatakwenda jela kutokana na muda ambao ameshautumikia kifungoni hapo awali. Mwanasiasa huyo alifutiwa mashtaka ya kutenda uhalifu wa kivita baada ya kukata rufani mnamo mwezi wa Juni, lakini alihukumiwa kwa mashtaka ya uzito wa chini ya kuvuruga ushahidi.
Hukumu hiyo ya jana inazizima kabisa jitihada za Bemba kugombea katika uchaguzi wa urais utakaofanyika mnamo mwezi Desemba katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambao tangu hapo alishazuiliwa na Tume ya Uchaguzi na Mahakama ya Katiba ya nchi yake.
Na Mary Mkeu.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

MAHAKAMA YA KIMATAIFA YAMHUKUMU BEMBA
Reviewed by By News Reporter
on
9/18/2018 07:30:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: