Loading...

AFRIKA KUSINI YAHALALISHA MATUMIZI YA BANGI

Loading...
Mahakama ya Kikatiba nchini Afrika kusini imehalalisha utumiaji wa bangi kwa watu wazima katika maeneo faragha.

Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo kwa kauli moja, kuruhusu watu wazima kutumia bangi wakiwa majumbani na kukuza kiasi kinachoweza kutosheleza mahitaji binafsi.

Wanaharakati wanaounga mkono utumiaji wa bangi wamesheherekea uamuzi huo wa kihistoria wakisema ''sasa tuko huru''.

Akitoa hukumu hiyo Naibu jaji Mkuu, wa Afrika Kusini, Raymond Zondo, amesema sheria inayopiga marufuku watu wazima kutumia bangi ilikuwa kinyume cha katiba.

Serikali ya Afrika kusini bado haijatoa tamko lolote kuhusiana na na uamuzi huo.

Watumiaji watatu wa bangi walikuwa wanakabiliwa na mashtaka walijitetea mbele ya mahakama hiyo wakisema '' mashataka dhidi yao yaliingilia uhuru wao''

Naibu jaji mkuu Raymond Zondo alisema: "Sio hatia kwa mtu mzima kutumia au kugusa bangi akiwa katika eneo la faraghani hasa ikiwa anafanya hivyo kwa maatumizi yake ya kibinafsi''

Licha ya uamuzi huo, ni hatia kwa mtu kuvuta au kuuza bangi hadharani.

Baraza la ukuzaji bangi nchini Afrika Kusini limeunga mkono uamuzi wa mahahakama dhidi ya matumizi ya bangi na kutoa wito kwa serikali kuwaondolea mashtaka watu waliyopatikana na kileo hicho.

Jeremy Acton, kiongozi wa chama cha Dagga, ambacho kinaendesha kampaini ya kuhalalishwa kwa matumizi ya bangi pia kimepongeza uamuzi huo wa mahakama ya katiba kimesema uamuzi huo pia ungelijumuisha kuhalalisha ubebaji wa bangi hadharani.

Bangi hutambuliwa kama "dagga"nchini Afrika Kusini.
Na Felista Julius.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
AFRIKA KUSINI YAHALALISHA MATUMIZI YA BANGI AFRIKA KUSINI YAHALALISHA MATUMIZI YA BANGI Reviewed by By News Reporter on 9/19/2018 06:40:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.