Loading...

VISA NA MIKASA: MCHUNGAJI AGOMA KUFANYA MAOMBI KWA UROHO WA SADAKA

Loading...
Ilikuwa sinema ya bure katika eneo la Nguni, Mwingi - Kenya huku mchungaji akiwashangaza wengi kwa kugoma kumuombea tajiri mmoja aliyemuita nyumbani kwake ili afanyiwe maombi.

Kulingana na habari hiyo ilichapishwa katika gazeti la Taifa Leo, tajiri huyo alimwalika mchungaji huyo amuombee kwa mema ambayo Mungu alikuwa amemtendea.

Kwa kuwa ana utajiri mkubwa, mchungaji huyo alifika nyumbani kwake upesi akiandamana na wazee wa kanisa akijua kuwa angepata sadaka nono. 

Mambo yalibadilika huku tajiri huyo akitoa sadaka ya ya Sh2500, jambo ambalo lilomkasirisha mchungaji huyo.

Badala ya kufanya maombi, mchungaji huyo aliwaamrisha waumini alioandamana nao kurudi makwao, jamblo lililomshangaza kibosile huyo. 

"Usiondoke bila kuombea familia yangu," jamaa alimsihi mchungaji.

Pasta huyo alifunguka na kumueleza kuwa maombi yanahitaji gharama na sadaka aliyotoa ilikuwa ndogo. Haikubanika kama jamaa huyo aliamua kuongeza sadaka au la.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
VISA NA MIKASA: MCHUNGAJI AGOMA KUFANYA MAOMBI KWA UROHO WA SADAKA VISA NA MIKASA: MCHUNGAJI AGOMA KUFANYA MAOMBI KWA UROHO WA SADAKA Reviewed by By News Reporter on 9/19/2018 07:02:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.