Loading...

MGANGA ASAKWA KWA MADAI YA 'KUFUNGA' MVUA

MGANGA mmoja aliyekuwa akihudumia eneo la Bungoma, Kenya alilazimika kujificha kwenye mapango baada ya wanakijiji kumvamia wakidai alikuwa amezuia mvua kunyesha.

Inasemekana mganga huyo kutoka taifa jirani alikuwa akidai kwamba alikuwa na uwezo wa kufanya mvua inyeshe au kuzuia isinyeshe.

Tetesi zinasema kwamba jamaa huyo alikuwa amehudumia mkazi mmoja aliyekataa kumlipa Sh85,000 kisha akatishia kufanya jambo ambalo wanakijiji wote wangejutia maishani mwao.

“Kama sitapata pesa zangu kwa muda wa siku saba, mjue kila mtu hapa atajuta. Sitaki kujua utatoa wapi pesa ila mimi ninataka kulipwa kabla ya juma kumalizika,’’ alitishia mganga huyo.

Inasemekana kiangazi kilianza kushuhudiwa eneo hilo huku wakazi wakishangaa tatizo lilikuwa nini. Wanakijiji walianza kushituka mazao yao yalipoanza kunyauka na kuharibika.

Hapo ndipo alipoanza
Loading...
ushukiwa kuwa ni mganga huyo ndio aliyekuwa chanzo cha masaibu hayo hasa kufuatia vitisho vyake baada ya kutolipwa deni.

Kulingana na msimuliaji, wanakijiji waliandamana hadi kwa mganga huyo wakiimba nyimbo za kumkejeli na kutishia kumpa funzo la mwaka.

Baada ya kupata fununu kwamba maisha yake yalikuwa hatarini, jamaa huyo alichomoka kupitia dirisha la nyuma na kutimua mbio kuelekea mapango yaliyo milimani. Wanakijiji walipofika kwake, hawakumpata kwani alikuwa tayari ametoroka ili kujihakikishia usalama wake na hatimaye kujificha kwenye mapango.

Wakazi hao waliapa kutumia njia zote kumsaka na kumpatia kipigo mganga huyo kwa kuwasababishia balaa.

"Hatutatulia wakati mtu anakuja hapa na kutuletea shida. Atakiona cha mtema kuni. Nimepoteza kila kitu shambani kutokana na ukosefu wa mvua. Hasara niliyopata ni zaidi ya Sh6.8 milioni," alisema mkulima mmoja.
Na Peter Godwin.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MGANGA ASAKWA KWA MADAI YA 'KUFUNGA' MVUA MGANGA ASAKWA KWA MADAI YA 'KUFUNGA' MVUA Reviewed by By News Reporter on 9/28/2018 09:29:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.