Loading...

TANZANIA YAIMARIKA SEKTA YA AFYA, YATUNUKIWA TUZO KIMATAIFA

SERIKALI ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepata Tuzo ya Kimataifa ya kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza (NCDs) kama vile Kisukari, Shinikizo la Damu, Magonjwa ya Moyo na Saratani.

Tuzo hiyo ya Kimataifa, imekabidhiwa jana tarehe 27 Septemba, 2018 kwa Waziri ya Afya Ummy Mwalimu na Kikosi kazi maalumu cha Umoja wa Mataifa mahususi kwa kupambana na Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (UN Interagency Task Force on the Prevention & Control of NCDs- UNIATF).

Hii ni kutokana na juhudi za Wizara ya Afya za kupambana dhidi ya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (NCD), hususani kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara.
Loading...
Tuzo hiyo ya kimataifa ya mwaka 2018, imekabidhiwa kwenye mkutano wa wa viongozi wa juu wa Umoja wa Mataifa (United Nations High Level Meeting on NCDs) unaofanyika Mjini New York, Marekani.

Timu ya UNIATF imeipongeza Tanzania kwa kuanzisha programu ya kuhamashisha jamii kufanya mazoezi kama sehemu ya maisha yao ya kila siku.

“ Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (NCD) ndiyo yanayoongoza duniani kwa sasa kwa kusababisha ulemavu na vifo vingi. Nchini Tanzania asilimia 34 ya Vifo vilivyorekodiwa Hospitali mwaka 2017 zimesababishwa na magonjwa haya. Isitoshe kupambana na NCD ni miongoni mwa mikakakati ya Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo Endelevu (SDG) ya kupunguza kwa theluthi moja vifo vya mapema vitokanavyo na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ifikapo mwaka 2030. Amesema Waziri Ummy.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
TANZANIA YAIMARIKA SEKTA YA AFYA, YATUNUKIWA TUZO KIMATAIFA TANZANIA YAIMARIKA SEKTA YA AFYA, YATUNUKIWA TUZO KIMATAIFA Reviewed by By News Reporter on 9/28/2018 08:52:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.