Loading...

MJI AMBAO NYUMBA HUJENGWA BILA MILANGO

Loading...
Shani Shingnapur ni mji mdogo wenye kaya (nyumba) zipatazo 200 katika wilaya ya Ahmednagar ya Maharashtra, India, ambako wengi wa waumini huenda kuabudu kwa mungu wa Hindu, Bwana Shani.

Ndani ya mji huo utapata hekalu za heshima zaidi za Mungu Shani za nchini India, na wakazi wa Shani Shingnapur wameweka imani juu ya mungu wao kama mlinzi wao. Kutokana na hadithi inayosimuliwa kwa miaka 300 iliyopita, hakuna nyumba katika kijiji ambayo ishawahi kuwa na mlango. Na imani hiyo inaenda mbali zaidi hadi katika majengo ya kibiashara na umma kama hoteli, benki na vituo vya polisi. Na hakuna duka lolote katika mji wa Shani Shingnapur linalouza kufuli na funguo.

Wakazi wa mji huo huenda katika shughuli zao za kiuchumi bila wasiwasi juu ya usalama wa nyumba zao na mali zao. Hiyo ni kwasababu ya imani yao imara ya Mungu Shani na wakati mwingine huenda hata safari za mbali bila kuwaambia majirani wachunge mali zao.

"Kama mtu atakosa uaminifu au kujaribu kuiba kijijini hapo, mtu huyo hataweza kukwepa adhabu ya Mungu Shani," alisema Dyaneshwar Kudalkar, ambaye anayemiliki biashara ya nyumba za wageni.

"Tunapolindwa kwa kiasi hiki, hatuhitaji kuwa na wasiwasi na kujiwekea ulinzi wa zaida. Kumekuwa na matukio kwa waliojaribu kuweka milango au miamba katika nyumba zao na wamepata matatizo, ajali na hasara katika biashara, hata kupata mikosi."

Shani, mji ambao unaaminika kuna usalama na imani ya hali juu, vituo vya polisi vimeanza kujengwa hivi karibuni mnamo mwaka 2015. Lakini mpaka kufikia 2010 hakukuwahi kupatikana taarifa yeyote ya uhalifu, lakini sasa kuna malalamiko kidogo kuhusu kuibiwa kwa sonara, pesa taslimu na baadhi ya vito vya thamani.

Kutokana na historia fupi ya mji huu, basi unaweza ukawa mji pekee salama nchini India.
Na Haika Gabriel.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MJI AMBAO NYUMBA HUJENGWA BILA MILANGO MJI AMBAO NYUMBA HUJENGWA BILA MILANGO Reviewed by By News Reporter on 9/15/2018 04:26:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.