Loading...
Mwandishi wa riwaya wa Oregon ambaye alikamtwa juma lililopita kwa mauaji ya mumewe alichapisha insha mtandaoni iliyoitwa 'Jinsi ya Kumuua Mume Wako,' imeripotiwa.
Nancy Crampton Brophy, 68, alikamatwa wiki iliyopita kwa mauaji ya Juni 2, ya Daniel Brophy.
Brophy mwenye umri wa miaka 63 alipigwa risasi hadi kufa ndani ya Taasisi ya Ufugaji ya Oregon huko Portland.
Mke wake, ambaye anaandika riwaya za mapenzi na riwa za mambo yaliyojificha, pia aliandika blogu kwenye WordPress kuhusu kumuua mwenza wake iliyowekwa kwenye Tovuti ya See Jane Publish.
Kwa sasa tovuti hiyo imezuiliwa na mmiliki peke yake ndio anaweza kutazama makala hiyo, lakini mashirika ya habari yalifanikiwa kupiga picha makala hiyo.
Crampton-Brophy alikamatwa Jumatano ya wiki jana huko nyumbani kwake kwa shutuma za kutekeleza mauaji ya mumewe katika Taasisi ya Ufugaji ya Oregon.
Crampton-Brophy - ambaye alichapisha riwaya aliyoiita 'The Wrong Husband' na 'The Wrong Lover' - yupo kizuizini chini vyombo vya usalama katika kata ya Multnomah kwa shutuma za mauaji na kutumia bunduki kinyume na sheria, kulingana na mtandao wa Oregon Live.
Crampton-Brophy amefunguliwa kesi ya mauaji na alifikishwa mahakamani Alhamisi mchana ya wiki jana, lakini haina uwakika kama atakuwa na mwanasheria mpaka sasa.
Na Paskali Joseph.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MWANDISHI WA INSHA 'JINSI YA KUMUUA MUME' MBARONI
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
9/13/2018 08:23:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: