Loading...

CARLOS TEVES AFICHUA TOFAUTI ILIYOPO KATI YA MESSI NA RONALDO

Loading...
Aliyekuwa mchezaji wa Manchester United na raia wa Argentina Carlos Tevez amefichua tofauti iliyopo kati ya Cristiano Ronaldo wa Ureno na mwenzake wa Argentina, Lionel Messi.

Kiu ya kumpata ni nani bora kati ya wawili hao imekuwa ikiuandama ulimwengu huku kila mchezaji akitoa mchango wake kwa suala nzima la uchezaji kwani wote wawili ni wababe katika fani ya soka.

Baada ya kucheza kwenye timu moja na wote wawili; Ronaldo wakiwa Manchester United na Messi katika timu ya kitaifa ya Argentina, Tevez alitoa tofauti anayohisi inatawala wawili hao katika fani ya soka. 

Kulingana na Tevez, hajawahi kumuona Messi akifanya zoezi kwa Gym ila amemuona Ronaldo mara nyingi.

Alisema kuwa kwa Messi, ni talanta kwani huwa hafanyi kazi ngumu ili kujipa nafasi hiyo katika ulimwengu wa soka. 

"Ni kawaida kwake, ila kwa penalti, alijifunza," Alisema kumhusu Messi. 

Alisema kwa kuwa Cristiano hutengeneza sana kipaji chake hata kufanya mazoezi kupita kiasi na kufika kazini mapema.
Na Hamisi Lukamba.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
CARLOS TEVES AFICHUA TOFAUTI ILIYOPO KATI YA MESSI NA RONALDO CARLOS TEVES AFICHUA TOFAUTI ILIYOPO KATI YA MESSI NA RONALDO Reviewed by GEOFREY MASHEL on 9/13/2018 08:38:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.