Loading...

GAVANA OBADO ANAYEHUSISHWA NA KIFO CHA MWANAFUNZI, AKANUSHA TUHUMA HIZO

Loading...
Gavana wa Migori Zachary Obado hatimaye amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya kuhusishwa na mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Rongo, Sharon Otieno.

Obado alituma rambi rambi zake kwa familia jamaa na marafiki wa Sharon Otieno huku akiyakana madai ya kuhusika kivyovyote katika kifo cha mwanafunzi huyo.

Akiwahutubia wanahabari kwa mara ya kwanza Jumatano, Septemba 12 tangu kuripotiwa kwa kifo cha Sharon, Obado alieleza kuwa suala hilo limeihangaisha familia yake vya kutosha.

Gavana huyo aliwaomba wanasiasa kukomesha uvumi kuhusu suala hilo na kuwapa maafisa wa polisi nafasi kufanya uchunguzi wao ili kubainisha kifo cha mwanadada huyo.

‘’ Naomba wanasiasa kukoma kuongea kiholela kuhusu suala hili. Sina uhusiano wowote na kifo cha Sharon. Naomba muwape wachunguzi nafasi kufanya kazi yao ili waliomuua Sharon kuchukuliwa hatua,’’ alisema. 

Obado alieleza kuwa alilazimika kuandamana na familia yake kutoa hotuba hiyo maana suala hilo limeihangaisha familia yake mno.

''Nina familia yangu hapa maana tumesongwa mno na suala hili, hata usingizi hakuna. Mimi ni mwananchi ninayeheshimu sheria na sikuhusika kivyovyote katika kifo cha Sharon. Nitasaidia kadri niwezavyo katika uchunguzi. Vitengo vyote vinavyohusika katika uchunguzi huo uongeze kasi,’’ aliongzea. 

Aidha aliishukuru familia yake pamoja na umma kwa jumla kwa kumpa moyo wakati huo mgumu.

Hapo awali iliripotiwa Gavana kuhusika na kifo cha mwanafunzi huyo, alipatikana kuuawa msituni baada ya kutafutwa kwa muda ambaye inasemekana alikuwa na mahusiano ya kimapenza na Obado na hata ujauzito aliokuwa nao tumboni uliwa wa mwanasiasa huyo maarufu.
Na Hamisi Fakhi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
GAVANA OBADO ANAYEHUSISHWA NA KIFO CHA MWANAFUNZI, AKANUSHA TUHUMA HIZO GAVANA OBADO ANAYEHUSISHWA NA KIFO CHA MWANAFUNZI, AKANUSHA TUHUMA HIZO Reviewed by By News Reporter on 9/13/2018 08:55:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.