Loading...
Jamaa mwenye umri wa makamo, katika eneo la Nguirubi, Limuru-Kenya aliwaacha maafisa wa polisi pamoja na umma kwa jumla vinywa wazi Jumatano, Septemba 12 baada ya kudai kuwa alikuwa ameagizwa na Mungu kukuza bangi kwa kiwango kikubwa.
Njoroge Mbugua aliwaambia maafisa wa polisi kuwa hajuti kufanya biashara hiyo maana ni wito wa Mungu.
Aliwashangaza zaidi maafisa hao alipowaambia kuwa alikuwa amesafiri hadi mbinguni kwa wakati moja na kuwa na kikao na Mungu kabla kurudi duniani.
‘’ Hata nikiacha biashara hii, ni Mungu aliyeniagiza kukuza bangi. Nimewahi kwenda mbinguni na kurudi duniani. Kuna watu wengi sana wanaoutumia mmmea huu,’’ alieleza.
Maafisa hao ambao walikuwa wamelivamia shamba hilo kubwa walichukua muda mrefu kuiondoa mimea hiyo na kuiweka katika gari lao.
Mbugua alikamatwa na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Tigoni baada ya maafisa polisi kupashwa habari na wachungaji wa ng’ombe kuhusu biashara hiyo.
Na Catherine Kisese.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
JAMAA ANAYEDAI KUAGIZWA NA MUNGU KULIMA BANGI MBARONI
Reviewed by By News Reporter
on
9/14/2018 08:03:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: