Loading...
Padri mmoja wa kanisa la Katoliki la Parokia ya Kipsania kaunti ya Trans Nzoia, Kenya alikamatwa na maafisa wa polisi baada ya kupatikana akimnajisi msichana mwenye umri wa miaka 11.
Kulingana na mama wa mwaathiriwa, padri Benard Magina Masinde alitekeleza kitendo hicho Septemba 15, 2018 ndani ya gari lake katika soko la Kipsaina kata ndogo ya Cherengany.
Mama huyo aliliambia gazeti la Daily Nation kwamba, alikuwa amemtuma mwanawe kununua mafuta ya taa sokoni mwendo wa saa moja jioni lakini alijawa na wasiwasi baada ya mwanawe kuchukua muda mrefu kurudi nyumbani.
Alimfuata hadi sokoni ambapo alimpata mwanaye ndani ya gari la padri huyo huku akiwa nusu uchi.
"Niliamua kumfuata mwanangu hadi sokoni nilikokuwa nimemtuma na la kushangaza, nilimkuta kwenye gari la padri huyo lililokuwa limeegeshwa kando ya barabara, nilipochungulia ndani nilimuona padri akiwa nusu uchi pamoja na mwanangu, nilizua rabsha papo hapo na maafisa wa polisi wakafika eneo la tukio na kumkamata" Mama mwaathiriwa alisema.
Masinde alifikishwa mbele ya hakimu Paul Mutai lakini alikana mashtaka dhidi yake na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh 6.7 milioni. Kesi hiyo itazikizwa tena Oktoba 1.
Na Mussa Rashid
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

PADRI MBARONI KWA KUMNAJISI BINTI MDOGO
Reviewed by By News Reporter
on
9/18/2018 06:50:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: