Loading...

RAPA KANYE WEST ABADILI JINA

Akitangaza kupitia mtandao wake wa Twitter siku ya Jumamosi, aliandika hivi: "Mtu aliyekuwa anajulikana Kanye West. Sasa anaitwa Ye."

West, 41, amekuwa akiitwa 'Ye' wakati mwingine kama jina lake la zaida na sasa ameitambulisha albamu yake ya nane na kuiita 'moniker' ambaye ameiachia rasmi mwezi Juni.

Mabadiliko hayo yamefanyika kabla ya kuonekana kwake Saturday Night Live, ambapo alitarajiwa kuzindua albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Yadhi.

Loading...
ans-serif;">Aliendelea kuelezea maana ya jina lake la Ye, West alisema hapo mwanzo neno hilo linamaana na umuhimu sana katika dini yake.

Ye inamaanisha 'wewe' akiendelea kufafanua alisema mimi ni wewe, mimi ni sisi. Alidai albamu yangu ya sasa ni kama inaelezea sisi tuyafanyayo.

Kanye amekuwa moja kati ya marapa maarufu waliowahi kubadili majina yao.

Sean Combs amejulikana kama Puff Daddy, P.Diddy or Diddy, lakini mwaka huu alitangaza pendekezo la kuitwa Love na Brother Love.
Na Jafari George.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
RAPA KANYE WEST ABADILI JINA RAPA KANYE WEST ABADILI JINA Reviewed by By News Reporter on 9/30/2018 06:59:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.