Loading...

RONALDO AKATAA SHUTUMA YA UBAKAJI

Cristiano Ronaldo ametupilia mbali madai ya mwanamke mmoja nchini Marekani ambaye anadai kuwa Ronaldo alimbaka mwaka 2009.

Kwenye video ya Instagram Ronaldo alisema: "Wanataka umaarufu kwa kutumia jina langu. Hiyo ni kawaida."

Mawakili wa Ronald wanasema wanalishtaki jarida la Ujerumani la Der Spiegel lililoripoti kwanza madai hayo.

Jarida hilo lilindika kuwa Kathryn Mayorga alikuwa amedai Ronaldo 33, alimbaka kwenye chumba kimoja cha hoteli huko Las Vegas.

Bi Mayorga, 34,
Loading...
anaripotiwa kuandika taarifa ya kubakwa kwa polisi wa Las Vegas muda mfupi baada ya kisa hicho.

Mwaka 2010 anaripotiwa kufikia makubaliano na Ronaldo ya malipo ya dola 375,000 ili asifichue madai hayo.

Mawakili wake sasa wanataka makubaliano y kutofichua madai hayo yatupiliwe mbali.

Ronaldo alijiunga na Juventus ya Italia kwa pauni milioni 99.2 akitokea Real Madrid mapema mwaka huu.

Mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Ureno anatajwa kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi kipindi hiki duniani.
Na Rehema Mussa.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
RONALDO AKATAA SHUTUMA YA UBAKAJI RONALDO AKATAA SHUTUMA YA UBAKAJI Reviewed by By News Reporter on 9/30/2018 06:43:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.