Loading...

SOUDY BROWN NA MAUA SAMA BADO HALI NI TETE

Loading...
Jumatatu ya jana watu wengi waikuwa wanahamu ya kujua hatma ya wapendwa wao maua sana na soudy brown kutokana na mahakama kusema kuwa kesi za watu hao zingeweza kusikilizwa jana jumatatu ya septemba 24.

Hata hivyo, Maua Sama hakupandishwa kizimbani kabisa huku Soudy Brown alipandishwa kizimbani na kusomewa mashataka ya kurusha video katika mtandao bila kuwa na kibali na hata dhamana ya kosa hili iko wazi lakini soudy ameshindwa kupewa dhamana kwa sababu kosa la pili linamfunga Soudy Brown kupata dhamana.

Hata hivyo kesi ya pili ya soudy brown inategemewa kusomwa October 18 mwaka huu huku maua kesi yake ikiwa haijasomwa kabisa ikisemwa kuwa kesi hiyo inaweza kusikilizwa katikati ya wiki hii.

Soudy na Maua walikamatwa wiki iliyopita huku kosa kubwa ikiwa ni kuweka video katika mitandao ya kijamii ikiwa na kosa la kudhihaki pesa ya Tanzania ambayo ilonekana ikikanyagwa na mashabiki wao katika wimbo wa Iokote, hata hivyo soudy bado anaonekana akiwa na kesi ya kujibu pia kwa kosa la kuanzisha Youtube channeli bila kibali cha TCRA.
Na Hamisi Abdallah.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
SOUDY BROWN NA MAUA SAMA BADO HALI NI TETE SOUDY BROWN NA MAUA SAMA BADO HALI NI TETE Reviewed by By News Reporter on 9/25/2018 08:19:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.