Loading...

T-SHIRT ZA MWANAMUZIKI WIZKID ZAVUNJA REKODI YA MAUZO

Loading...
Nyota wa muziki wa Afro pop, Ayodeji Balogun a.k.a Wizkid anang'ara duniani kwa sasa na flana zake mpya zilizobuniwa na kutengenezwa na kampuni maarufu ya nguo za michezo ya Nike, zimeuzwa zote baada ya uzinduzi.

Staa huyo alitangaza uzinduzi wa t-shirt zake kupitia mtandao wake wa Instagram, na punde akatangaza flani hizo zimeuzwa zote kwa muda wa dakika 10.

Kulingani na Nike, ushirikiano wa utengenezwaji wa flana za Wizkid ni sherehe ya mafanikio ya safari ya muziki ya msanii huyo anayefanya vizuri Nigeria na dunia ki ujumla.

Flana hizo nembo ya STARBOY imechorwa mbele yake na mikononi kumewekwa rangi ya kijani na nyeupe kuashiria mahali alipotokea wizkid, aliripoti mwanahabari wa Nigeria.
Na Geofrey Okechi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
T-SHIRT ZA MWANAMUZIKI WIZKID ZAVUNJA REKODI YA MAUZO T-SHIRT ZA MWANAMUZIKI WIZKID ZAVUNJA REKODI YA MAUZO Reviewed by By News Reporter on 9/14/2018 12:58:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.