Loading...
Mtengenezaji filamu wa nchini Kenya, Wanuri Kahiu ameendelea kupambania filamu yake ipate kibali cha kuonyeshwa katika nchi yake.
Filamu ya RAFIKI inayoelezea mahusiano ya jinsia moja kati ya wasichana wawili, imepata umaarufu mkubwa tangu ilipozinduliwa rasmi katika tamasha la filamu huko Cannes, Ufaransa mapema mwaka huu na kuifanya Kenya kuwa nchi ya kwanza kufanya hivyo kwa barani Afrika.
Hata hivyo, Bodi ya Uainishaji wa Filamu ya Kenya ilipiga marufuku filamu hiyo, ikisema kwamba "inataka kuhalalisha mapenzi ya jinsia moja na vitendo vya ushoga."
Kahiu kupigania filamu yake ionyeshwe nchini humo bado hakujakoma, baada ya kutangaza wiki hii TIFF kwamba yeye na wasanii wenzake wamefungua mashtaka ili kuishtaki bodi hiyo ya filamu.
Shtaka hilo linataka marufuku iliyopigwa dhidi ya filamu hiyo kuperekwa mbele ili Tuzo za Oscar ziweze kumfikiria au kumuweka kwenye vipengele vya tuzo hizo. Pia kutoa msukumo ili kubadilisha sheria ambayo imetumiwa kupiga marufuku filamu maarufu na katuni kama Wolf ya Wall Street na Adveture Time.
"Mimi sijichukulii kuwa ji mwanaharakati; kwa dhati najichukulia ni mwandishi wa simulizi," Kahiu alisema TIFF. "Lakini mtu anapoanza kuchukua haki zako za kuunda ubunifu na kufanya kazi yako, inakuwa tatizo. Hapo ndipo tulipoamua kuifikisha Bodi ya Uainishaji wa filamu mahakamani."
Kwa RAFIKI kustahili tuzo bora ya Lugha za Kigeni, inahitaji kuonyeshwa nchini Kenya kabla ya Septemba 30, Ripota wa Hollywood aliongezea. Kama kamati ya uteuzi itapewa ruhusa ya kuicheza filamu hiyo na kuiwasilisha katika Chuo, RAFIKI itakuwa filamu ya kwa ya Wakenya kuteuliwa katika kipengele hicho.
"Sio haki kwa serikali kusema nini unaweza kufikiri na nini hauwezi kufikiria," Kahiu anaongeza. "Na anayetakiwa kuwepo. Hiyo sio njia ambayo unaweza kuendesha nchi, kwa sababu tumezaliwa na watu tofauti."
Na Neema Bushubo.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

MTAYARISHAJI WA FILAMU YA 'RAFIKI' KUISHTAKI BODI YA FILAMU YA KENYA
Reviewed by By News Reporter
on
9/14/2018 10:46:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: