Loading...

WALIOMTIA PILI PILI MTOTO SEHEMU ZA SIRI MAHAKAMA YAWAPATIA HUKUMU

Loading...
Mahakama ya Wilaya ya Kusini Makunduchi Unguja jana imewatia hatiani watu watatu na kuwaamuru walipe shilingi millionI moja kwa kila mmoja kwa kosa la shambulio la aibu kwa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 17.

Waliohukumiwa kulipa faini ni Salma Abdallah Zahor (43) Mkaazi wa Kizimkazi Mkunguni, Hamida Hassan Khamis (34), Mkaazi wa Fuoni na Asha Kombo Ali (65) Mkaazi wa Kizimkazi Mkunguni wote kwa pamoja wametakiwa kulipa fedha hizo.

Aidha mahkama hiyo imewataka akina mama hao wote watatu wamlipe fidia ya laki tano mtoto waliyemdhalilisha, kila mmoja, fedha ambazo atapewa muhanga moja kwa moja.

Tukio la mtoto huyo wa miaka 17 lilitokea Tarehe 10 mwezi wa 11 mwaka 2017, Watu hao walishitakiwa na kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria ya adhabu namba 6 ya mwaka 2004 kifungu 131 cha Sheria za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Imedaiwa kwamba mnamo tarehe 10 majira ya saa 1 usiku akina mama hao watatu walitwanga pilipili, chumvi, kitunguu na thomu na baadae kumtia katika sehemu zake za siri wakiamini kuwa inapunguza kufanya hamu ya mapenzi, ambapo walidai kuwa mtoto huyo amekuwa akifanya mapenzi.

Hata hivyo kwa mujibu wa uchunguzi na maelezo ya daktari hatua hiyo ilimsababishia maumivu makali mtoto huyo na kumuathiri ambapo sehemu zake za siri zilionekana zimevimba ana kutokana na maumivu hayo.

Akizungumza nje ya Mahakama Mama wa mtoto huo alisema awali walikwenda kwenye kituo cha polisi kushitaki baada ya kumuona mtoto wake ametendewa jambo hilo na kumuona mwanawe ameumia.

Hata hivyo kesi hiyo iliyofunguliwa Novemba mwaka jana wa 2017.
Na Neema Joshua.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
WALIOMTIA PILI PILI MTOTO SEHEMU ZA SIRI MAHAKAMA YAWAPATIA HUKUMU WALIOMTIA PILI PILI MTOTO SEHEMU ZA SIRI MAHAKAMA YAWAPATIA HUKUMU Reviewed by By News Reporter on 9/14/2018 08:38:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.