Loading...
Mwanamume mmoja katika eneo la Port Harcourt, Nigeria alikamatwa katika kanisa la kianglikana la St. Mark’s akijaribu kuiba sadaka.
Habari hizo zilichapishwa mtandaoni na mtumiaji wa Facebook kwa jina Ezekiel West Tamunominabo aliyefichua kuwa alinaswa akijaribu kufungua sanduku hilo la fungu la kumi kwa kutumia waya.
Kulingana na Ezekiel, mwanamume huyo aliweza kuiba Naira 500 (sawa na Sh 3900 pesa za Tanzania) kutoka kwenye sanduku hilo.
Alisema kuwa mhubiri wa kanisa hilo alimwombea mwizi huyo baada ya kuhojiwa na waumini wa kanisa hilo waliomfumania akitekeleza kitendo hicho.
Kwenye chapisho hilo la Facebook, ilibainika kuwa jamaa huyo amekuwa akiendeleza tabia hiyo kwa muda katika makanisa kadhaa eneo hilo.
“Mapema leo asubuhi katika kanisa la kianglikana la St. Mark’s, mwanamume alikamatwa akiiba pesa kutoka kwenye sanduku la fungu la kumi altareni. Alipata Naira 500 kutoka kwenye sanduku hilo. Baada ya uchunguzi, mwanamume huyo amekuwa akitekeleza wizi huo katika makanisa mjini humo kwa kutumia waya na pipi mpira kufungua sanduku hilo ambalo hufungwa kwa kufuli.
“Msimamizi wa kanisa hilo alimwombea mwanamume huyo aliyedai kuiba kwenye kanisa hilo mara kadhaa. Wanasema siku moja kwa mwizi na siku moja kwa mmiliki,” Ezekiel Tamunominabo aliripoti.
Na Fatma Pembe.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

VISA NA MIKASA: JAMAA AKAMATWA AKIIBA SADAKA KANISANI KWA KUTUMIA WAYA
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
9/05/2018 10:33:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: