Loading...
Mwanamume, 20, anayetokea Kaunti ya Meru, Kenya amekamatwa baada ya kumteka mwanafunzi wa darasa la nane na kumnyanyasa kingono mtoto huyo kwa siku tatu.
Mwirigi Kimathi Jumanne, Septemba 11, alikutwa akiwa na hali mbaya baada ya wakazi kuripoti kisa hicho kwa maafisa wa polisi.
Kulingana na wazazi wa msichana huyo, alipotea Ijumaa Septemba 7. Na siku tatu zimepita mpaka walipogundua alikokuwa, kulingana na KNA, Jumatano, Septemba 12.
Msichana huyo mwenye miaka 14 ni mwanafunzi katika shule ya msingi Kaunti Ndogo ya Igembe Central.
Akithibitisha kisa hicho, msimamizi wa kituo cha polisi eneo hilo Joseph Merigchan, alisema uchunguzi unaendelea na kwamba mshukiwa alikuwa amezuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Maua.
Visa vya unyanyasi wa kingono kwa watoto vimeongezeka eneo hilo na wakazi wamezitaka taasisi husika kuchukua hatua madhubuti dhidi ya wahusika.
Afisa wa watoto eneo hilo, John Mwangi, alisema watoto wanahitajika kulindwa dhidi ya wanajisi.
Na Leornard John.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
VISA NA MIKASA: MWANAUME ALIYEMTEKA MWANAFUNZI NA KUMNAJISI MBARONI
Reviewed by By News Reporter
on
9/14/2018 02:03:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: