Loading...
Upepo mkali unaotokana na Kimbunga Florence ambacho kinatishia watu wengi Marekani kimeanza kupigia maeneo ya pwani ya mashariki ya Marekani.
Maafisa wameonya kwamba huenda mawimbi makubwa ya kutoka baharini na mvua kubwa vikaathiri maeneo ya North na South Carolina, huku kimbunga hicho kikielekea maeneo ya bara.
Upepo wa kimbunga hicho unavuma kwa kasi ya maili 100 kwa saa (155 km/h).
Nyumba takriban 100,000 tayari hazina huduma ya umeme huku hali ikitarajiwa kuwa mbaya zaidi.
Maafisa wa serikali wametahadharisha kwamba kimbunga hicho kinaweza "kuwaua watu wengi sana" huku kukiwa na wasiwasi wa kutokea mafuriko "mabaya sana".
Watu zaidi ya milioni moja katika maeneo ya pwani North Carolina, South Carolina na Virginia walikuwa wametakiwa kuyahama makazi yao.
Maelfu walitafuta hifadhi katika vituo vya muda vya huduma za dharura Alhamisi usiku.
Na Peter Samwel.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
KIMBUNGA CHA FLORENCE CHAANGAZIWA KUUA WENGI MAREKANI
Reviewed by By News Reporter
on
9/14/2018 02:27:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: