Loading...

WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA UINGEREZA 'TONY BLAIR' KUGOMBANIA UONGOZI EPL

Loading...
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair ametajwa kuwa ni mwenyekiti mtarajiwa wa Ligi ya Premier, Uingereza 

Wengine walioko katika kinyang’anyiro hicho ni aliyekuwa mkuu wa BT Gavin Patterson na msimamizi wa Sky Sports Barney Francis.

Kulingana na Dailymail, waziri mkuu huyo wa zamani alitajwa wakati wa mazungumzo yasiyo rasmi wakati wa mkutano wa klabu hiyo wiki jana.

Mwenyekiti wa sasa Richard Scudamore, aliushtua ulimwengu alipotangaza kuwa angejiuzulu baada ya miaka 20 kusimamia ligi hiyo kama mwenyekiti.

Blair, ambaye ni shabiki sugu wa Newcastle United alikuwa akitaka kuunganisha Ligi ya Uingerea na Scotland alipokuwa waziri mkuu kati ya 1997-2007.

Ikiwa atachaguliwa, kiongozi huyo aliye na miaka 65 atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa kuna maadili katika klabu 20 za hadhi ya juu EPL.

Gordon Taylor, mkurugenzi mkuu wa chama cha wachezaji wa kulipwa wa kandanda hata hivyo alionya kuwa atakayechukua mahali pa Scudamore atakuwa na kibarua cha kulinda kilichoanzishwa na Scudamore. 

"Tunatarajia kufanya uteuzi unaostahili katika muda unaostahili ili kusiwe na matatizo wakati wa mpito,” alisema Taylor.

"Ninazungumzia klabu zote ninaposema tunahuzunika kwamba Richard anaondoka, lakini hatungeomba zaidi kutoka kwake, kwa miaka 20, ameongoza Premier League vizuri,” alisema.
Na Paskali Joseph.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA UINGEREZA 'TONY BLAIR' KUGOMBANIA UONGOZI EPL WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA UINGEREZA 'TONY BLAIR' KUGOMBANIA UONGOZI EPL Reviewed by By News Reporter on 9/20/2018 09:38:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.