Loading...

BAADA YA BOBI WINE, MSANII MWINGINE ADAKWA NA POLISI

Loading...
Mwanamuziki mkongwe, Viboyo Oweyo - kwa jina halisi - Moses Nsubuga amekamatwa na polisi kwa madai ya kutoa wimbo uliomtusi Rais Yoweri Museveni na Spika wa Bunge, Rebecca Kadaga.

Kwa mujibu wa Vincent Ssekatte, msemaji wa Idara ya Uchunguzi wa makosa ya Jinai, Viboyo alitumia maneno machafu kushambulia viongozi wa serikali na hivyo anashikiliwa na polisi katika Kituo cha Polisi cha Jinja Road akikabiliwa na kesi ya shambulizi la lugha chafu.

Polisi pia wanadai kuwa Viboyo alisema kwamba ameshoshwa na uongozi wa nchi ya Rwanda, kwa kumshutumu kufanya mauaji ya msemaji wa polisi wa zamani Andrew Felix Kaweesi na Andrea Kayiira.

Tukio hili linafuatia baada ya majuma kadhaa kupita tangu sakata la Bobi Wine ambaye ni msanii na mbunge, kukamatwa na afisa usalama wa Uganda na kuteswa hadi kufikia kuperekwa nje kwa matibabu. Vuguvugu la kisiasa katika ya makundi ya wasanii dhidi ya viongozi wa nchi hiyo inaanza kukua kadri siku zinaposonga.
Na Owino Otuma.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com 
BAADA YA BOBI WINE, MSANII MWINGINE ADAKWA NA POLISI BAADA YA BOBI WINE, MSANII MWINGINE ADAKWA NA POLISI Reviewed by By News Reporter on 10/06/2018 10:50:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.