Loading...

TAARIFA KWA UMMA: MATIBABU MAPYA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

Napenda kuwataarifu kuwa hivi karibuni, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeanzisha utoaji wa huduma za tiba radiolojia(interventional radiology) inayohusisha utaalam wa kutumia vifaa vya radiolojia kama MRI, CT-Scan, Ultra-Sound na X-RAY kutibu moja kwa moja au kuchukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi.

Tayari tumeanza kuondoa uvimbe kwenye sehemu ya kinywa, uso na shingoni (sclerotherapy forhaemangioma and lymphangioma),kuweka mirija kwenye figo ambazo mirija ya kutoa mkojo imeziba(nephrostomy tube placement), kuzibua mirija ya nyongo iliyoziba(percutaneous trans hepatic biliary drainage) na kuzibua mirija ya uzazi iliyoziba(fallopian tube recanalization). Tiba nyingine ni kunyonya usaha ndani ya tumbo(abscesses drainage)

Kutokana na mafanikio hayo, napenda kuwataarifu kuwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) pamoja na Chuo Kikuu cha Yale kilichopo nchini Marekani tumeandaa kambi maalumu ya kufanya uchunguzi na kutoa tiba radiologia kuanzia tarehe 22 Oktoba hadi 9 Novemba 2018, hivyo tunaomba mtume wagonjwa wenye matatizo yafuatayo:

  • Lung abscess/nodules/masses
  • Uvimbe / majipu kwenye mapafu
  • Liver abscesses/nodules/masses
  • Uvim
Loading...
e / majipu kwenye ini
  • Kidney abscesses/nodules/masses
  • Uvimbe /majipu kwenye figo
  • Biliary system obstruction with dilatation
  • Mfumo wa nyongo ulioziba
  • Renal obstructive uropathy with severe hydronephrosis
  • Mfumo wa mkojo ulioziba
  • Abscesses/ collections anywhere (abdominal/pelvic/peritoneal)
  • Uvimbe /majipu ndani ya tumbo na nyonga


  • Gharama za Matibabu!
    Wenye bima za afya waje nazo,wasiokuwa na uwezo tutawapa exemption. Kumbuka kuwapa barua za rufaa waje nazo.

    Imetolewa na
    Aminiel Aligaesha
    Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja
    Hospitali ya Taifa Muhimbili

    Na Mussa Ibrahim.


    Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
    TAARIFA KWA UMMA: MATIBABU MAPYA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI TAARIFA KWA UMMA: MATIBABU MAPYA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI Reviewed by By News Reporter on 10/06/2018 12:19:00 PM Rating: 5

    Hakuna maoni:

    Inaendeshwa na Blogger.