Loading...

MAAJABU YA DUNIA: KICHWA CHA MAREHEMU CHATOWEKA, MAZISHI YAAHIRISHWA

Loading...
Familia moja kutoka kaunti ya Narok nchini Kenya iliahirisha mazishi ya ndugu yao baada ya kutoona kichwa chake kilichodaiwa kutoweka.

Inasemekana ni kinyume na tamaduni za jamii ya Wamaasai kumzika mtu bila viungo vyote vya mwili.

Kulingana na taarifa za gazeti la The Standard, familia ya marehemu ilikuwa tayari imechanga pesa za kugharamia hafla ya mazishi iliyotarajiwa kufanywa jana Ijumaa Oktoba 5.

Maafisa wa polisi wanasemekana kupata mwili wa Robert Chepkwony kwenye shamba la mahindi na kuupeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti.

Wazee wa jamii ya Wamaasai waliwarai maafisa wa polisi kutafuta kichwa cha marehemu ndipo waweze kumzika ila hakijapatikana hadi leo.

Chepkwony mwenye umri wa miaka 33 alifariki hivi majuzi kutokana na shambulizi la Olposimoru lililosababishwa na ufukuzwaji wa wakazi katika msitu wa Mau. 

Chifu wa eneo hilo Benjamin Maritim alisema kuwa familia ilifanya ushawishi wa kutosha na baadaye kukubaliana na kisa hicho.

"Wazee wa jamii ya Wamaasai walikutana na familia ya marehemu na baada ya majadiliano, hafla ya mazishi iliahirishwa. Inasemekana masaibu/mikosi yanaweza kuikumba familia hiyo iwapo marehemu atazikwa bila kichwa," Maritim alisema. 

Maritim alisema kuwa iwapo kichwa cha marehemu hakitapatikana basi itailazimu familia kufanya tambiko kabla ya kuendelea na mazishi.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MAAJABU YA DUNIA: KICHWA CHA MAREHEMU CHATOWEKA, MAZISHI YAAHIRISHWA MAAJABU YA DUNIA: KICHWA CHA MAREHEMU CHATOWEKA, MAZISHI YAAHIRISHWA Reviewed by By News Reporter on 10/06/2018 12:56:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.