Loading...
Msanii Wema Sepetu ameitwa na kuhojiwa na Bodi ya Filamu kufuatia picha na video zake zenye maudhui ya kingono, kusambaa mitandaoni.
Akizungumza na EATV, Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza, amesema kwamba msanii huyo amevuka kiwango cha uhayawani, na kutaka mtu au taasisi yoyote kutofanya kazi na msanii huo.
Pia Katibu huyo wa BASATA amezungumzia juu ya msamaha aliouomba jana muigizaji Wema Sepetu, na kusema kuwa ni unafiki mkubwa kwani sio mara ya kwanza wala ya pili kwake.
“Hii ni kama unafiki fulani, kwa sababu hii sio mara ya kwanza kwa msanii huyu, wala sio mara ya pili, na niseme tu kwamba kwa upande wa Baraza lina mchango wake kufikia hapo alipofikia, ile ni unafiki, haitoshi, mtu mara ya kwanza ya pili unasema hii ni tabia zake, na kwa vile kuna sheria zingine zilizovunjwa, lazima wahusika wachukue hatua zake, hii haitoshi, lazima awe mfano”, ameongeza.
Hapo jana msanii Wema Sepetu aliitisha mkutano na waandishi wa habari kuomba msamaha kwa tukio lake la udhalilishaji na kuaibisha la kusambaa kwa video yake chafu ya ngono.
Msanii mwingine anayelengwa ni Amber Ruti, japo Naibu Waziri, Juliana Shonza amesema mpaka sasa BASATA haimtambui kama msanii. Pia amehaidi kukomeshwa kwa tabia hizo chafu.
Na Richard Vincent.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

BODI YA FILAMU YAMFUNGIA WEMA SEPETU MOJA KWA MOJA, KUFUATIA SAKATA LA PICHA ZA KINGONO
Reviewed by By News Reporter
on
10/26/2018 04:13:00 PM
Rating:
![BODI YA FILAMU YAMFUNGIA WEMA SEPETU MOJA KWA MOJA, KUFUATIA SAKATA LA PICHA ZA KINGONO](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhmvaWdCA0PI6yKmaXcGpNNzK4MSTr-5ShRn0kMTqS8jzig1C3UA9egc8fuKjH3wtR-bWECF8Rgeow2xOIkyIiKRE16-D1lKb9FGNnBbYYo5B2zuGt_9Ao2G6T08VA31Fme_STqP4ouCnk/s72-c/wema+kufungia+na+bodi+ya+filamu+siku+zisizo+julikana.jpg)
Hakuna maoni: