Loading...

FACEBOOK YADUKULIWA, MKURUGENZI MKUU ATHIBITISHA

Facebook imetangaza Ijumaa kuwa takribani akaunti milioni 50 zilidukuliwa na wadukuzi kutokana na makosa ya kiusalama.

Mtandao huo mkubwa wa kijamii umesema kuwa uligundua mashambulizi ya akaunti za wateja wao wiki iliyopita, kwamba wadukuzi waliiba tokeni mahususi kama funguo zinazotumika kuingilia katika akaunti za wateja wao.

"Ni dhahiri kwamba wadukuzi walipata ruhusa ya kubadili mwenendo wa programu ya Facebook," Makamu rais wa usimamizi wa bidhaa Guy Rosen alisema katika chapisho la Blogu.

"Tumetatua tatizo la uvamizi na tumetaarifu vyombo vya usalama."

Mkurugenzi Mkuu wa Facebook Mark Zuckerberg alisema wahandisi waligundua udukuzi huo Jumanne, na kuuzuia siku ya Alhamisi usiku.

"Hatujafahamu kama kuna akaunti yeyote imeathiriwa," Zuckerberg alisema. "Hili ni swala zito."

Kwa tahadhari, Facebook kwa muda imezuia kipengele cha "View as" --- ikielezewa kama kipengele cha fa
Loading...
agha kinachomuwezesha mtumiaji wa mtandao kujiona anavyoonekana na marafiki wake.

"Tunakabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa watu ambao wanataka kuchukua akaunti za watu na kuiba taarifa za watu duniani kote," Zuckerberg aliyasema hayo kwenye ukarasa wake wa Facebook.

"Ingawa nafurahi tumeliona hili mapema, tumesahihisha uvamizi huu, na tukalinda akaunti ambazo zilikuwa hatarini, uhalisia ni kwamba tunahitaji kuendelea kubuni njia mpya ya kuzuia hili lisitokee tena."

Facebook imesema ilichukua hatua ya ziada kwa wale wate walioathiriwa, ambazo ni akaunti karibia milioni 40, waliondolewa (Logout) katika akaunti zao na walilazimika waingie upya (login).

Rosen alisema: "Faragha na usalama wa watu ni muhimu sana, na tunasikitika kwa tukio hili kutokea."

Udukuzi wa faragha za watumiaji wa mtandao wa Facebook umekuwa ni kitendo cha aibu kwa sasa, ambapo mapema mwaka huu ilikubali kwamba zaidi ya watumiaji milioni 10 walidukuliwa data zao na kampuni ya kisiasa iliyokuwa ikifanya kazi na rais Donald Trump wa Marekani mwaka 2016.
Na Geofrey Okechi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
FACEBOOK YADUKULIWA, MKURUGENZI MKUU ATHIBITISHA FACEBOOK YADUKULIWA, MKURUGENZI MKUU ATHIBITISHA Reviewed by By News Reporter on 10/01/2018 10:03:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.