Loading...
Jana Oktoba 5 mwaka 2018 msanii muziki wa kizazi kipya, Nasseb Abdul maarufu Diamond amevunja ukimya kwa kutaja siri iliyomfanya afanikiwe kwenye muziki wa Bongo Fleva.
Wakati Diamond anataka kutaja siri iliyomfikisha katika kilele cha mafaniko mamia ya wananchi wa Tandale, viongozi wa ngazi wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na wageni waalikwa walikuwa kimya.
Diamond alianza kueleza hatua kwa hatua sababu ambazo zimemfanya awe na mafanikio katika maisha yake ni siri kubwa ya kufanikiwa kwake anasema hachagui kazi ya kufanya.
"Katika maisha yangu sijawahi kuchagua kazi ya kufanya. Ndio maana kwenye maisha yangu nimefanya kazi nyingi sana.Nimefanya kazi ya kuuza mafuta sheli.nimefanya kazi ya kupiga picha kwenye kumbi za harusi pamoja na nimefanya kazi ya kuuza nguo Tandale.
"Siri nyingine ni kujenga uaminifu kwa watu ambao unafanya nao kazi. Uaminifu umenisaidia sana na ndio maana leo niko hapa,"amesema Diamond.
Amesema siri nyingine ni ubunifu na kufafanua baada ya kufanya kazi kwa bidii aliamua kuwa mbunifu kwa kila alichokuwa akikifanya.
Pia amesema kuomba Mungu ni jambo la msingi sana na katika maisha yake moja ya jambo ambalo lazima alifanye ni kumuomba Mungu na amemsadia kumfikisha hapo alipofika.
"Nimekuwa nikimuomba Mungu anisaidie katika shughuli zangu za muziki .Napoomba nataja kabisa kile ambacho nahitaji ili kumrahisisha Mungu kile ambacho nahitaji kwake.Sitaki kumchanganya kwa kuomba mambo mengi.
"Leo hii nimefanikiwa kwasababu namshikirisha Mungu,"amesema Diamond na kuongeza kuwa kwa anayetaka kufanikiwa lazima ajiepushe na matumizi ya dawa za kulevya.
Na Nassib Hatibu.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

HATIMAYE DIAMOND AFICHUA SIRI ALIYOHIFADHI KWA MUDA MREFU
Reviewed by By News Reporter
on
10/06/2018 06:42:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: