Loading...
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda jana ametangaza kuondoa muda wa Kikomo kwa wasanii kupiga mziki kwenye matamasha hadi Saa sita usiku Na sasa amewaongezea muda hadi Saa nane usiku kwa siku za weekend pekee.
Hatua hiyo imepokelewa kwa shangwe na wasanii nchini ambao kilio chao kilikuwa kuongezewa muda wa kufanya matamasha ili waweze kujipatia kipato cha kujikimu kimaisha kuendana na kaulimbiu ya Rais wao Mpendwa Dkt. John Magufuli inayowataka watu kufanya kazi.
Hii pia ni matokeo ya kuimarika kwa ulinzi na usalama wa jiji hilo la kibiashara na ongezeko la Kumbi nyingi zinazozuia kelele kutoka nje (soundproof) ambapo lengo la RC Makonda ni kuona siku moja watu wanafanya shughuli za kibiashara kwa Saa 24.

Na Neema Bushubo.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
HATIMAYE RC MAKONDA AONGEZA MUDA WA KUPIGWA MUZIKI DAR
Reviewed by By News Reporter
on
10/06/2018 06:34:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: