Loading...

TAARIFA KWA UMMA: TANGAZO LA KUITWA KAZINI

Loading...
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) inapenda kuwatangazia waombaji kazi wa nafasi mbalimbali za kada za Afya walioomba kazi kuanzia tarehe 10/05/2018 hadi tarehe 25/05/2018 kuwa mchakato wa kuwapangia vituo vya kazi umekamilika kwa awamu ya pili. Awamu hii ni kwa ajili ya kujaza nafasi wazi za Watumishi waliopangiwa katika awamu ya kwanza ambao hawakuripoti katika muda uliopangwa.

Waombaji wote waliopangiwa vituo vya kazi wanatakiwa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

i) Kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa kuanzia tarehe 20/10/2018 hadi tarehe 01/11/2018. Aidha, waombaji watakaoshindwa kuripoti kwenye vituo vya kazi ndani ya huo muda nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine haraka iwezekanavyo.

ii) Kuwasilisha vyeti halisi (Originals Certificates) vya kidato cha nne, sita, chuo, NACTE na vyeti halisi vya usajili wa mabaraza ya kitaalamu kwa ajili ya kuhakikiwa na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira. Waombaji wenye transcript na wasio na vyeti halisi pamoja na leseni hawatapokelewa.

iii) Hakutakuwa mabadiliko ya vituo kwa namna yoyote ile, hivyo
atakaoshindwa kuripoti katika vituo walivyopangwa, nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine wa kada husika.

iv) IIi kuepuka usumbufu, waombaji wote waliopangiwa vituo wanatakiwa kuzingatia vyeo walivyopangiwa kwenye orodha wawe na vielelezo vyote kabla ya kwenda kuripoti katika kituo husika.

Waombaji wote ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili, watambue kuwa hawakupata na£asi hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.

Waajiri wote mnaelekezwa kuwapokea, kuhakiki vyeti na kuwafanyia mafunzo elekezi (Induction Course) kabla ya kuwapangia vituo vya kazi.

Orodha ya majina ya waliopangiwa vituo vya kazi inapatikana kupitia tovuti ya OR-TAMISEMI www.tamisemi.go.tz.

Limetolewa na:-

Mathew Kwembe
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
OR - TAMISEMI

05/10/2018

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
TAARIFA KWA UMMA: TANGAZO LA KUITWA KAZINI TAARIFA KWA UMMA: TANGAZO LA KUITWA KAZINI Reviewed by GEOFREY MASHEL on 10/06/2018 06:22:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.