Loading...

IDADI YA WALIOFARIKI NA MAPOROMOKO YA UDONGO WAFIKIA 50 UGANDA

Loading...
ZAIDI watu 50 wamepoteza maisha kutokana na maporoko ya ardhi na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha mashariki mwa Uganda.

Mamia ya watu bado hawajulikani walipo huku maofisa katika wilaya ya Bududa wakihofu kuwa idadi ya waliopoteza maisha huenda ikaongezeka. Walioshuhudia mkasa huo wanasema kuwa mwamba ulidondoka mtoni na kupasua kingo za mto hali iliyosababisha maji yaliyochanganyikana na matope kuanza kusomba watu vijijini.

Serikali imesema vikosi vya uokoaji vimepelekwa katika eneo hilo karibu na mpaka wa Uganda na Kenya lakini miundo mbinu ya barabara na daraja iliyoharibiwa imekwamisha shughuli za uokozi. 

Maporomoko mengine ya udongo yaliyoshuhudiwa katika eneo hilo la Bududa yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 300 mwaka 2010.

Kufuatia ttukio la mwaka 2010,  wakazi wa sehemu hiyo waliiamriwa kuhama eneo hilo lakini wengi wao walirejea kwa kuvutiwa na ardhi yenye rutuba na upendo wa makazi yao ya asili.
Na Warrid Tumaini.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
IDADI YA WALIOFARIKI NA MAPOROMOKO YA UDONGO WAFIKIA 50 UGANDA IDADI YA WALIOFARIKI NA MAPOROMOKO YA UDONGO WAFIKIA 50 UGANDA Reviewed by By News Reporter on 10/13/2018 10:42:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.