Loading...
- Nyoka mmoja alizua hali ya taharuki kwenye hafla iliyohudhuriwa na Rais Yoweri Museveni baada ya kutambaa kwenda alikokuwa amesimama rais huyo akihutubia.
- Walinzi wa rais Museveni waliwahi na kumuua nyoka huyo na hatimaye hutuba ikaendelea.
- Rais Museven alikuwa mtulivu kipindi chote mpaka kuuliwa kwa nyoka huyo.
- Huenda Museveni ana historia na nyoka, labda kutokana na wakati wake wa kupigana na serikali akiwa mwituni, kwa sababu alishauliwa chatu mkubwa shambani mwaka mwaka 2016.
Ziara ya Rais Yoweri Museveni katika kijiji cha Kirangira, wilaya ya Mukono nusura ikatizwe baada ya nyoka kutambaa kuja kwenye zulia nyekundu la rais.
Museveni alikuwa ameanza kuzungumza na wakazi kuhusu kwa nini serikali yake ilipinga polisi kuwafurusha watu kwa lazima kwenye ardhi ya Kirangira wakati jiko hilo asiyetarajiwa alipozua hali ya taharuki.
Iliripotiwa kuwa Museveni aliwasili Ijumaa, Oktoba 26 jioni kwa kuchelewa kukiwa na giza kwenye hema lake ingawa watu walikuwa na mwangaza.
Ghafla alitokea nyoka, walinzi wake waliomuona nyoka huyo na walichukua hatua ya haraka na kumgonga mnyama huyo kichwani.
Huenda Museveni ana historia na nyoka, labda kutokana na wakati wake wa kupigana na serikali akiwa mwituni.
Kwa mfano, mwaka wa 2016, maafisa wa polisi waliokuwa wakililinda boma la Museveni walilazimika kumpiga risasi chatu mkubwa aliyeingia kwenye shamba lake.
Kulingana na afisa wa polisi, chatu huyo aliyekuwa na kilo 80 na urefu wa futi 20 aliingia kwenye shamba la Museveni eneo la Kisozi, wilaya ya Gomba kwa nia ya kuwashambulia ng’ombe wake.
Afisa huyo alisema kuwa walijaribu kumshika nyoka huyo lakini alikuwa na vurugu, hali iliyowalazimu kumpiga risasi mara tatu na kumuua.
Na Fatma Pembe.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
JOKA LAZUA TAHARUKI MKUTANO WA MUSEVENI
Reviewed by By News Reporter
on
10/28/2018 08:50:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: