Loading...

KANISA KATOLIKI LAHIMIZWA KUTIZAMA UPYA SWALA LA USEJA NA UBASHA

Loading...
Mshauri wa juu wa Papa Francis ameonya Ijumaa kuwa Kanisa Katoliki liko hatarini kuingiliwa zaidi na polisi na serikali ikiwa halitashughulikia kashfa za unyanyasaji wa kingono kwa mapadri kwa kufanya mageuzi makubwa.

Kardinali Reinhard Marx ametoa wito wa kuwa na "mjadala wa wazi" ndani ya Kanisa Katoliki kuhusu ubasha, matumizi mabaya ya mamlaka na "useja na mafunzo ya upadri" kama sehemu ya muitikio kwa kadhia za ukiukaji wa kingono.

"Ikiwa hakuna hatua za kurekebisha zitakazochukuliwa na Kanisa -- na tunafanyia kazi hilo, tunapaswa kulifanyia kazi ---serikali haitakuwa na njia nyingine zaidi ya kuigilia," alisema Marx siku ya Ijumaa, akizungumzia uchunguzi unaoendelea dhidi ya viongozi wa Kanisaa katika mataifa kama Chile, Marekani na kwingineko.

Marx, mmoja kati ya washauri tisa wa kipadri wa papa Francis, alitoa matamshi yake katika uzinduzi wa shahada ya uzamili kuhusu ulinzi wa watoto katika chuo kikuu cha kichungaji cha Gregorian mjini Roma, ambako majesuti wanafundishwa. Uzinduzi wa kozi hiyo umekuja wakati Vatican imewakusanya mapadri zaidi ya 250 kujadili namna ya kuboresha uchungaji kwa vijana.
Na Geofrey Okechi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KANISA KATOLIKI LAHIMIZWA KUTIZAMA UPYA SWALA LA USEJA NA UBASHA KANISA KATOLIKI LAHIMIZWA KUTIZAMA UPYA SWALA LA USEJA NA UBASHA Reviewed by By News Reporter on 10/07/2018 05:50:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.