Loading...
Maafisa watatu wa Elecom, taasisi ya kuendesha uchaguzi wa rais nchini Cameroon wameuawa katika eneo la Bafut lenye wazungumzaji wengi wa lugha ya Kiingereza ambalo linapigania kujitenga.
Kumekuwa kukitokea mapigano ya mara kwa mara baina ya maafisa usalama na watu wanaopigania kujitenga katika eneo hilo na taarifa zinasema kuwa watu wenye silaha wamevamia na kushambulia kwa silaha maeneo ya karibu na vituo vya kupigia kura.
Taarifa hizo zimeongeza kuwa, watu wawili wanaopigania kujitenga na Cameroon wamepigwa risasi na maafisa wa polisi ya Cameroon na kuuawa. Uchaguzi wa rais wa Cameroon ulifanyika jana Jumapili tarehe 7 Oktoba, 2018. Wagombea 9 wamechuana kwenye uchaguzi huo akiwemo rais wa hivi sasa Paul Biya.
Watu wanaozungumza Kiingereza ambao wanapigania kujitenga na Cameroon walikuwa wametangaza kuwa hawatoruhusu kufanyika uchaguzi huo katika eneo lao.
Takwimu zinaonesha kuwa, tangu mwishoni mwa mwaka jana 2017 hadi hivi sasa, zaidi ya askari 30 wa serikali wameuawa katika mashambulizi ya watu wanaotaka kujitenga huko kusini magharibi mwa Cameroon. Makumi ya watu wamejeruhiwa katika kipindi hicho.
Baadhi ya vyama vya upinzani viliungana siku moja kabla ya uchaguzi huo ili kupambana na Rais Paul Biya mwenye umri wa miaka 85 na ambaye yuko madarakani kwa karibu miaka 36 sasa. Jana rais huyo aligombea tena urais kwa muhula wa saba wa kipindi cha miaka saba madarakani.
Na George Vitalis.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

MACHAFUKO YA UCHAGUZI CAMEROON, WATU WATANO WAUAWA
Reviewed by By News Reporter
on
10/08/2018 06:28:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: