Loading...

WAZIRI UMMY: MIUNDO MBINU YA AFYA SASA KUZIDI KUIMARIKA

Loading...
Serikali imekataa kupandisha hadhi kituo cha Afya kibaoni hospitali ya wilaya, badala yake imeziagiza halmashauri zote wilayani Kilomabero, kutenga maeneo kwa ajili ya kujenga kwa ajili ya kujenga hospitali za wilaya.

Kauli hiyoilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alipozungumza na watumishi wa kituo cha Afya kibaoni, mjini Ifakara.

Waziri Ummy alisema kutokana na kupanuka kwa wilaya hiyo na kuwa na halmashauri mbili za Wilaya ya Kilombero na Mji Ifakara na ongezeko la watu, huduma za afya zinatakiwa kupanuliwa, hivyo serikali imeamua kila halmashauri kujenga hospitali ya wilaya.

"Japo viongozi wa wilaya watajisikia vibaya kutokana na kauli hii, nimeona ni muhimu kituo hicho kiendelee kutoa huduma kama kituo cha afya na halmashauri ya mji itenge eneo lingine tayari kwa ujenzi wa hospitali ya wilaya ili kupanua huduma kwa wananchi," alisema.

Waziri huyo alisema hospitali hizo zitakapokamilika, wataletwa madaktari na wauguzi kwa kuwa baada ya uhakiki wa watumishi, kinachofanyika sasa ni kuboresha miundombinu katika sekta ya Afya.

Alisemaa serikali inatoa fedha nyingi katika sekta ya afya, ikiwemo katika kituo cha afya Kibaoni, kwa kuwa mwaka 2015 hadi 2016, zilikuwa zinatolewa sh. milioni 12, lakini tangu mwaka jana, fedha zimeongezwa hadi kufikia sh. milioni 137.

Waziri huyo aliwataka watumishi wa kada mbalimbali katika sekta hiyo, kubadilika na kuwatumia wana Kilombero kwa kufanya kazi kwa maadili na wale wachache ambao sio waaminifu, wabadilike.

Pia, aliwaagiza waganga wakuu wote wa halmashauri hizo. kuhakikisha rufaa zote zinazotoka katika vituo vya afya, zinapelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Francis, kwa kuwa serikali
inatoa sh. bilioni mbili za watumishi, sh. milioni 200 za dawa.

Waziri Ummy aliagiza watumishi 12, waliopelekwa katika hospitali hiyo ya rufaa, warudishwe katika Kituo cha Afya lfakara, kutokana na kuwa na upungufu wa watumishi wakati hospitali hiyo ya rufaa ina watumushi wengi wanaolipwa na serikali.

Awali, katika kikao hicho, watumishi walimweleza Waziri Ummy, changamoto wanazokumbana nazo  ikiwemo mlundikano mkubwa wa wagonjwa, kukosa gari la kubebea wagonjwa, kukosa jengo la utawala na kutolea dawa na upungufu wa madaktari na wauguzi.
Na Jimmy Luoga.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com
WAZIRI UMMY: MIUNDO MBINU YA AFYA SASA KUZIDI KUIMARIKA WAZIRI UMMY: MIUNDO MBINU YA AFYA SASA KUZIDI KUIMARIKA Reviewed by By News Reporter on 10/08/2018 07:32:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.