Loading...

MCHUNGAJI AFARIKI AKIMUOMBEA DUA MAREHEMU

Loading...
Mchungaji wa Kanisa la EAGT la walokole, lililoko Mji wa Sirari, Tarafa ya Ichungu, Wilayani Tarime, mkoani Mara, Nestory Papaa, amefariki wakati akimwombea marehemu katika mji wa kechanja, nchini Kenya.

Inaelezwa kwamba mchungaji huyo alikwenda huko na rafiki zake kuhani msiba wa jamaa ya rafiki yake.

Wakizungumza na gazeti moja hapa nchini, mwishoni wa wiki iliyopita, wakati wa mazishi ya mchungaji Papaa, Diwani wa kata ya sirari, ambaye pia ni mwenyekiti wa Kijiji cha Mpakani, Nyangoko Paulo na ndugu wa marehemu, Charles Papaa, walisema mchungaji huyo na rafiki zake, walikwenda kehancha, Jumatano ya wiki iliyopita.

"Nestory, ambaye ni kaka yangu, alikuwa mchungaji wa Kanisa la EAGT Walokole, lililoko Sirari na pia ni mfanya biashara wa duka la kuuza vipodozi. Jumatano walikwenda na rafiki zake, akiwemo Nyangoko Roman, kuhani msiba wa shemeji yake Roman, huko Kehancha, Kenya.

"Wakati akihubiri kwa kutoa neon, ghafla alizidiwa, akaishiwa nguvu na kuanguka. Rafiki zake walijitahidi kumpeleka hospitali ya Migoro kwa ajili ya kupatiwa matibabu, lakini alipoteza maisha," alisema Charles.

Mdogo wa marehemu, Charles, Mchungaji mwenzake, Baraka na Diwani wa kata ya Sirari, Nyangoko, walisema kifo cha mchungaji huyo hakipaswi kuhusishwa na imani za kishirikina kwa sababu siku inapofika, hakuna mwenye uwezo wa kukizuia kifo.

Charles alisema kaka yake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo na alifariki kutokana na ugonjwa huo.

Mazishi ya mchungaji huyo, yalifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, katika Kitongoji cha Buriba, kata ya Sirari.
Na Hatibu Hamadi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MCHUNGAJI AFARIKI AKIMUOMBEA DUA MAREHEMU MCHUNGAJI AFARIKI AKIMUOMBEA DUA MAREHEMU Reviewed by By News Reporter on 10/08/2018 08:35:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.