Loading...
JESHI la Polisi Mkoa wa Manyara linamshikilia mwalimu Charles Merikiory (32), wa Shule ya Msingi ya Rift Valley English Medium, wilayani Babati kwa kosa la kumlawiti mwanafunzi wa darasa la tano.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Augustino Senga, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Alisema tukio hilo lilitokea Septemba 28, mwaka huu majira ya saa 7:00 mchana katika shule hiyo iliyopo Mtaa wa Mruki.
Alidai mwalimu huyo alimlawiti mwanafunzi huyo baada ya kumdanganya na kumwingiza kwenye bweni la wavulana wakati wanafunzi wengine wakiendelea na vipindi vya dini.
Mwanafunzi huyo hakuwa anaishi kwenye mabweni kama ilivyo kwa wanafunzi wengine.
Aidha, Kamanda Senga alisema, chanzo cha unyama huo ni tamaa za kimwili na kingono na akawataka wazazi kuwa karibu na watoto wao kwa kuwauliza maendeleo yao wanapotoka shule.
Alisema kujulikana kwa tukio hilo kulitokana na taarifa zilizotolewa na mama wa mwanafunzi huyo alipotoa taarifa kituo cha polisi baada ya kusimuliwa mkasa mzima na mtoto wake.
Alisema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mama huyo walimfikisha hospitali kwa uchunguzi zaidi na Kamanda Senga alisema uchunguzi ulithibitisha mtoto huyo alilawitiwa.
Alisema ili kukomesha vitendo vya namna hiyo alitaka jamii kushirikiana kwa kutoa taarifa pale matukio kama hayo yanapotokea.
Kwa upande wake, Mkuu wa shule hiyo, Daelly Wilfred, alisema hizo bado ni tuhuma na hivyo hawezi kulizungumzia.
Hata hivyo, alisema madai ya kuwapo kwa tukio kama hilo ni la kwanza kutokea shuleni hapo.

Na Frank Malogo.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

MWALIMU MBARONI KWA TUHUMA ZA ULAWITI
Reviewed by By News Reporter
on
10/08/2018 09:13:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: