Loading...

RAPA KANYE WEST KUFANYA KAZI ZAKE AFRIKA

Loading...
Baada ya kiza kingi kutanda juu ya kuchelewa utambulishwaji wa albamu mpya ya Kanye West. Lakini rapa huyo alikuwa na sababu za msingi kueleza kwanini albamu yake haitozinduliwa siku ya Jumamosi.

Akifanya mahojiano na mtandao wa TMZ mubashara ambapo aliahidi kufafanua sababu iliyomfanya abadili siku iliyopangwa kuzindua album yake hiyo mpya, alisema sababu ya kuchelewa kuzindua albamu ambayo imeshika vichwa vya habari sasa ni kwa sababu anaelekea Afrika kutengeneza nyimbo kadhaa.

Alisema kwamba atadhuru huko kwa wiki chache kwa sababu anataka kuweka nguvu fulani juu ya kazi zake.

Na jina la nchi ambayo ataitembelea bado hajalitaja mpaka sasa! Na kinachofahamika mpaka sasa ni tarehe ya uzinduzi wa albamu hiyo mpya ya Yandhi ambayo itakuwa tarehe 23 Novemba.
Na Ummy Selemani.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
RAPA KANYE WEST KUFANYA KAZI ZAKE AFRIKA RAPA KANYE WEST KUFANYA KAZI ZAKE AFRIKA Reviewed by By News Reporter on 10/08/2018 09:48:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.