Loading...
Maelfu ya Wakenya wanaoishi kando ya Pwani wanaweza kulazimika kuhama miaka 20 ijayo kwa kuongezeka kwa maji yanayosababishwa na ongezeko la joto duniani.
Ripoti iliyotolewa leo inasema kuwa urefu wa usawa wa bahari unaongezeka kila uchwao kwa sababu dunia imeshindwa kudhibiti joto kupanda. Inakadiriwa kuongezeka kwa 1.5 sentigredi kulinganisha na joto la kawaida.
"Kote duniani, watu masikini wanatarajiwa kupata athari za ongezeko la joto la 1.5 sentigredi kwa kuongezeka bei za vyakula, usalama wa chakula na njaa, kupoteza mapato, kupoteza fursa za maisha, athari za afya na makazi ya watu," rasimu ya ripoti inasema.
Ripoti ya mwisho itafunguliwa nchini Korea Kusini leo na Jopo la Serikali za Mitaa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa - kikundi cha watafiti wa hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa.
Ripoti hiyo haikutaja Kenya kwa jina lakini, imethibitisha tafiti kadhaa ambazo zinaonyesha maeneo mengi ya Pwani, ikiwa ni pamoja na sehemu za jiji la Mombasa, ikionyesha uwezekano wa kuzama miji hiyo ifikapo mwaka 2040 ikiwa hali ya joto itaendelea kupanda zaidi. Kupashwa kwa joto kwa dunia kunapelekea kuyayuka kwa mabarafu makubwa yaliyoganda hiyo maji kuongezeka baharini na kufunika nchi kavu.
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

RIPOTI UN: MIJI YA PWANI AFRIKA MASHARIKI HATARINI KUPOTEA
Reviewed by By News Reporter
on
10/08/2018 11:03:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: