Loading...

MTANZANIA ASHINDA TUZO UMOJA WA MATAIFA

Loading...
Mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake na watoto kutoka nchini Tanzania Rebeca Gyumi, pamoja na wenzake watatu wameshinda tuzo ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka huu wa 2018.

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Maria Fernanda Espinosa, kupitia ukurasa wake wa Twitter amewapongeza kwa mchango wao wa kusongesha mbele haki za binadamu.

Rebeca na washindi wengine watatu wa mwaka huu watapatiwa tuzo yao mjini New York, Marekani tarehe 10 Desemba mwaka huu, wakati wa kilele cha tamko la haki za binadamu la umoja wa mataifa ambalo mwaka huu linatimiza miaka 70.

Mshindi mwingine ni Asma Jahangir mwanaharakati na mwanasheria wa Pakistani ambaye amefariki dunia mwaka huu.

Tuzo hiyo ilianza kutolewa mnamo mwaka 1973 na hadi leo imetolewa mara 10.
Na Ujugu Michael.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MTANZANIA ASHINDA TUZO UMOJA WA MATAIFA MTANZANIA ASHINDA TUZO UMOJA WA MATAIFA Reviewed by By News Reporter on 10/29/2018 04:42:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.