Loading...

SAKATA LA KUTEKWA MO, MPAKA SASA MAMBOSASA AFUNGUKA HAYA

Loading...
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amenukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema watuhumiwa wanaoshikiliwa kwa ajili ya kuhojiwa kutokana na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mo Dewji wamefikia 12.

Bw Dewji bado hajulikani alipo baada ya kutekwa mapema asubuhi ya jana jijini Dar es Salaam.

Kamanda Mambosasa alisema: “Dewji bado tunaendelea kumfuatilia na kuwafuatilia watu waliofanya uhalifu huo, wa kumteka.

“Zipo taarifa mtaani kwamba ameshapatikana, wengine wanadai kwamba amepatikana kule Coco Beach lakini taarifa kutoka meza yangu hii, na taarifa ambazo sasa ni taarifa rasmi, bado hajapatikana wala wahusika bado hawajakamatwa.

“Jeshi la polisi linaendelea na operesheni kali kufuatia tukio hilo, mikoa yote mitatu tunaendelea na ufuatiliaji wa karibu ili kuhakikisha kwamba tukio hili ambalo ni la aina yake na ambalo limefanywa na raia wa kigeni halipati nafasi ya kuchafua taswira nzuri ya Tanzania kwa maana ya mahali ambapo wahalifu, vinaendelea kukemewa kwa pamoja.

“Mahali ambapo watu wameendelea kuita ni kisiwa cha amani.”
Na Hashimu Ramadhani.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
SAKATA LA KUTEKWA MO, MPAKA SASA MAMBOSASA AFUNGUKA HAYA SAKATA LA KUTEKWA MO, MPAKA SASA MAMBOSASA AFUNGUKA HAYA Reviewed by By News Reporter on 10/12/2018 09:16:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.